YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Kijana aitwaye SIJAWA BAKARI (30) mkazi wa kijiji cha Nangumbu, Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, ameuawa kikatili kwa kukatwa Koromeo na watu wenye hasira kali baada ya kumtuhumu kuwa ni mwizi wa mazao ya wakulima mashambani. 

Picha ya Maktaba

Inaelezwa kuwa, kijana huyo alikuwa na Tabia ya wizi ambapo mwezi Mei, Mwaka huu ametoka jela baada ya kutumikia kifungo kwa wizi wa korosho mashambani. 

Kutokana na zao la ufuta kuongezeka bei hadi shilingi 4000/= kwa kilo, wezi wanaohujumu mazao ya wakulima shambani wamekithiri jambo ambalo linasababisha kuwepo kwa matukio mengi ya wizi na mauwaji katika msimu huu. 

Wananchi wanasimulia kwamba, walifahamu mienendo ya kijana huyo na kuamua kumfuata hadi nyumbani kwake ambapo walimkuta na shehena ya ufuta, licha ya yeye kutokuwa na shamba lolote. 

Wananchi wanasema kwamba, kijana huyo alikuwa akivamia mashambani na kuiba masuke ya ufuta na baadaye kwenda nayo nyumbani ambapo alikamatwa akiwa anakafua ufuta huo (kutoa ufuta kwenye masuke yake).

Post a Comment

Previous Post Next Post