YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa (kushoto) akiwasili ofosi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga (Kulia)

Japan kupitia Balozi wake nchini Tanzania Yasushi Misawa imeahidi kushirikiana na serikali ya mkoa wa Lindi katika kuliongezea thamani zao la ufuta Pamoja na uboreshwaji wa huduma ya afya ya mama na mtoto ikiwa ni miongoni mwa malengo yaliyowekwa na Taifa hilo kupitia mradi wa JICA ambao umekuwa ukifanya kazi mkoani Lindi kwa takribani miaka mitano iliyopita ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Sokoine.  

Balozi wa Japan nchini Tanzania Yasushi Misawa (kushoto) akioneshwa maeneo yenye madini mkoani Lindi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack (Kulia)

Balozi Yasushi Misawa ameambatana na Bi. Eri Ogawa ambaye ni Afisa ubalozi wa Japan katika ziara ya siku moja leo tarehe 15 Juni, 2023 kwa mwaliko wa mkuu wa mkoa huo Bi. Zainab Telack.  

Balozi Yasushi Misawa alipotembelea ghala la ufuta 'Moledina' lililopo manispaa ya Lindi

Bi. Telack akizungumza na vyombo vya Habari baada ya kikao cha mapokezi ya wageni hao amesema Japan kupitia mradi wa JICA wako tayari kushirikiana na serikali ya mkoa katika kukuza nyanja mbalimbali za kiuchumi ikiwemo uvuvi, kilimo cha mwani, uchimbaji wa madini na kilimo cha umwagiliaji ambapo tayari wameanza kufanya utekelezaji katika wilaya ya Nachingwea, Ruangwa, Liwale na maeneo ya Makangaga, Kinyope na Likunja.  

Balozi Yasushi Misawa akiwa katika maeneo tofauti ndani ya viunga vya Chuo cha Ufundi Stadi VETA - Lindi

Balozi Yasushi Misawa akiwa katika ghala la ufuta, Moledina lililopo manispaa ya Lindi amehoji ni kwa namna gani wakulima hupata malipo kutoka kwa wanunuzi pamoja na njia zinazotumika kupima ubora wa ufuta ambapo Majid Myao ambaye ni Katibu Tawala msaidizi, Uchumi na Uzalishaji ameeleza hatua mbalimbali zinazotumika kuanzia hatua ya ukusanyaji mpaka mauzo na hatua ya malipo kwa wakulima.  



Aidha Balozi Misawa ameshukuru kwa mwaliko na ameeleza furaha yake ikiwa ni kwa mara ya kwanza anatembelea mkoa wa Lindi na kupendezwa na mandhari yake. Pia ameeleza utayari wake wa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Lindi na Kitaifa ili kuendeleza, kudumisha na kulinda mahusiano kati ya taifa la Tanzania na Japan.

Post a Comment

Previous Post Next Post