Wachimbaji wadogo wa madini Mkoani Lindi wamepatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwenye masuala mbalimbali ikiwemo sheria ya madini ili kuwasaidia katika shughuli zao.

Na Elizabeth Msagula




Kwa mujibu wa Afisa madini Mkoa wa Lindi Emmanuel Shija mafunzo hayo yamehusisha wachimbaji wadogo wa madini na wazalishaji wa chumvi kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Lindi na Mkoa wa jirani wa Mtwara.

Akizungumza baada ya kufungua mafunzo hayo,Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amewataka wanufaika wa mafunzo hayo kuhakikisha wanakwenda kuyafanyia kazi mambo yote watakayopata kupitia mafunzo hayo huku pia kuwa mabalozi kwa wengine ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maonesho ya madini na fursa za uwekezaji yajulikanayo kama Lindi Mining Expo 2025 yanayoendelea Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi yaliyozinduliwa jana Juni 11 na kutamatika juni 14,2025.

Post a Comment

Previous Post Next Post