Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Lindi limetoa rai kwa wananchi wa Mkoa huo kuacha matumizi ya kuni na mkaa na badala yake watumie vifaa vya umeme vya kisasa katika kupikia na ambavyo havitumii umeme mwingi.

Na Elizabeth Msagula



Meneja wa Mkoa wa Lindi wa Shirika hilo Theodory Hall ametoa rai hiyo leo juni 12,2025 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack walipotembelea katika banda la Shirika hilo katika maonesho ya pili ya madini (Lindi Mining Expo 2024 yanayoendelea Wilayani Ruangwa.


Hatua hiyo ni katika kuhamasisha mkakati wa serikali wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ambao unalenga ifikapo mwaka 2034, kila Mtanzania awe anatumia nishati safi, salama na nafuu kwa ajili ya kupikia.

Meneja Theodory Hall amesema Wizara ya Nishati imetoa kibali kwa wasambazaji wazawa katika kuuza vifaa hivyo nchini kote kwa bei ya ruzuku ambapo kwenye maonesho hayo wanashirikiana nao  kuelimisha jamii juu ya matumizi ya nishati safi kwa kuhakikisha wanatumia vifaa vya umeme vya kisasa kama pressure cooker, na majiko ya umeme ambayo yanatumia umeme mdogo kwa matumizi ya majumbani.

Post a Comment

Previous Post Next Post