Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC kimechapisha ripoti mpya ya hali ya haki za binaadamu kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki kwa mwaka uliopita. Ripoti ya aina hiyo hutolewa kila mwaka kuangazia hali ya haki mbalimbali ikiwemo za kisiasa na kijamii. 

Picha ya Maktaba

Utafiti huo uliofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) umeonesha kuwa, Watoto ndio waathirika wakubwa wa matukio yaliyoripotiwa na kurekodiwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Tanzania kwa (47%), wakifuatiwa na wanawake (33%), wazee (10%) na Watu wenye Ulemavu (4%). 

Kwa mujibu wa ripoti ya LHRC iliyozinduliwa Jumatano Aprili 12, 2023 jijini Dar es Salaam, 6% iliyobaki walikuwa waathirika wengine, ikiwa ni pamoja na wanachama wa vyombo vya kutekeleza sheria. Mwaka 2022, LHRC iligundua angalau matukio 350 dhidi ya watoto yaliyoripotiwa Tanzania Bara, huku ukatili wa kijinsia ukichukua sehemu kubwa (asilimia 81) ya matukio hayo. 

Robo (asilimia 25) ya wahathiriwa walikuwa chini ya umri wa miaka kumi, huku wavulana wakiwa ndio wengi (asilimia 78) ya waathiriwa wa kulawiti.

Post a Comment

Previous Post Next Post