Wananchi katika tarafa mbili za milola na Nangaru, jimbo la Mchinga halmashauri ya Manispaa ya Lindi wamerahisishiwa   mawasiliano, na usafirishaji wa mazao na bidhaa kutoka tarafa hizo kwenda barabara kuu ya Lindi -Dar es Salaam. 


Na E. Msagula

Hiyo ni baada ya wakala wa barabara za mijini na Vijijini TARURA kuwajengea daraja lenye upana wa mita 15.60 katika barabara ya Chikonji-Nangaru -Milola na hivyo kuondoa adha waliokuwa wanaipata kwa kipindi cha miaka 15 ya kusafirisha mazao yao kutokanana na eneo hilo kujaa Maji na kutopitika vizuri hasa wakati wa mvua. 

Daraja hilo limezinduliwa Leo Aprili 13, 2023 na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 ABDALLAH SHAIB KAIM Mara baada ya kulikagua na kujiridhisha juu ya utekelezaji wake ambapo ametumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa tarafa hizo kukumbuka shida walizopata kwa miaka 15 na hivyo iwalazimu kutohujumu miundombinu ya daraja hilo ili iweze kudumu na kuendelea kuwanufaisha. 

Wananchi wa Milola na Nangaru wakiongozwa na mbunge wa Mchinga SALMA RASHID KIKWETE wamemueleza kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kuwa, daraja hilo litainua uchumi kwani kwa sasa watakuwa na uwezo wa kuvuka hata wakati wa mvua na watatembeleleana na kusaidiana kibiashara. Kwa mujibu wa Meneja wa TARURA mkoa, Mhandisi DAWSON PASCHAL mradi huo umekamilika kwa asilimia 100 na kugharimu kiasi cha shilingi Milioni 778,665,000.00/=

Post a Comment

Previous Post Next Post