Wafanyabiashara wa soko kuu la Samaki Lindi wamelalamikia uongozi wa manispaa ya Lindi kutoboresha soko hilo licha ya kutoa ushuru wa asilimia tatu kwa kila bidhaa wanayochukua.

Eneo la Mnada, Soko la Samaki Manispaa ya Lindi

Wafanyabiashara hao wamesema ukubwa wa soko hilo haufanani na maeneo mengine kwani maeneo mnada  wa Samaki unapofanyika, meza zake si rafiki na hata eneo la kuuzia Samaki halipo sawa licha ya kulalamika kwa muda mrefu.

Meza za Biashara, Soko la Samaki Manispaa ya Lindi

Mwenyekiti wa soko hilo Naibu Masela amesema kama uongozi waliwahi kufuatilia kwa kupeleka barua bandarini mkoa wa Mtwara ambayo ilienda makao makuu na majibu yalipotoka waliambiwa wanaweza kupatiwa eneo na baada ya kupeleka majibu hayo halmashauri ya manispaa ya Lindi, hawakupatiwa majibu mpaka leo.

Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa, wafanyabiashara wapo tayari kuhamishwa popote na wanatamani wahamishiwe eneo la #Names Lindi mjini. Lakini walipoonesha uongozi wa halmashauri eneo hilo, walikataa kujenga ikiwa bado wanaendelea kuchukua ushuru katika biashara yao. 

Muonekano wa Mbele Soko la Samaki Manispaa ya Lindi

Baada ya kupokea kero hizo na kuzifikisha ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Lindi, Juma Mnwele, amewaomba viongozi wa soko la samaki kufika ofisi za halmashauri kwa mazungumzo zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post