YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Majongoo Bahari (Picha na SJMC - UDSM)

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi David Silinde amezitaka halmashauri zilizopo ukanda wa pwani kutoa kipaumbele kwa mikopo kwa vijana waliopatiwa mafunzo ya ukuzaji na ufugaji wa majongoo bahari ili kuongeza mapato.

Hayo ameyasema wakati wa hafla ya ufungaji na ugawaji wa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya ukuzaji na ufugaji wa majongoo bahari mkoa wa Lindi yaliyoongozwa na wakala wa elimu na mafunzo ya uvuvi FETA ambapo takribani watu wapatao 68 wamepatiwa mafunzo hayo.

Silinde amesema asilimia kubwa ya halmashauri za kanda ya pwani mapato yao ni madogo hivyo ni vyema wakiwekeza kwenye ufugaji wa majongoo wa bahari na rasilimali za bahari ili kuleta mapato makubwa katika halmashauri hizo huku akizitaka kuwahamasisha wanawake na vijana katika shughuli hizo na kuwa endelevu.

Awali mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, amesema endapo nguvu kubwa itawekezwa katika uzalishaji wa mazao ya bahari ikiwemo kuhusisha idadi kubwa ya vijana na wanawake, basi itasaidia kukua kwa mapato katika mkoa wa Lindi na kuondoa changamoto za kiuchumi zilizopo kama inavyofanyika katika zao la mwani ambapo mkoa wa Lindi ni miongoni mwa wazilishaji wakubwa wa zao hilo.


Post a Comment

Previous Post Next Post