YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW



Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Ashatu Kijaji amesema wizara hiyo itashughulika na sheria zote zinazokwamisha utendaji katika biashara, viwanda na uwekezaji.

Ameyasema hayo hii leo mkoani Njombe kwenye mkutano wa saba wa baraza la biashara la mkoa wa Njombe ambalo limehusisha wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali kwenye mkoa huo.

Awali mwenyekiti wa wafanyabiashara taifa Hamisi Livembe ameeleza kuhusu changamoto ya ushuru wa huduma namna unavyoleta mkanganyiko kwa wafanyabiashara nchini. Livembe amebainisha kuwa tatizo la ushuru huu ni pale inapokosa maelezo kwani inasemwa kuwa ni kodi ya huduma huku huduma zote zikilipiwa tofauti.

Aidha amesema wafanyabiashara hutozwa ushuru wa taka, OSHA na kadhalika na kupendekeza kuwa kodi hiyo ifutwe ama ipewe jina jingine kulingana na huduma hali itakayoepusha migogoro.

Post a Comment

Previous Post Next Post