YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW




Baraza la Wawakilishi nchini Marekani lenye mpasuko mkubwa limetumbukia katika mzozo kwa siku ya pili mfululizo jana baada ya duru mpya za upigaji kura kushindwa kumpata mshindi wa kinyang'anyiro cha uspika

Warepublican katika Baraza la Wawakilishi walishindwa kwa siku ya pili mfululizo kumchagua kiongozi, wakati kundi la wahafidhina chamani likiendelea kukaidi wito wa Rais wa zamani Donald Trump wa kuungana nyuma ya mshirika wake Kevin McCarthy.

Baada ya kushindwa katika duru tatu za upigaji kura na mikutano kadhaa ya faragha, McCarthy alionekana kuwa mbali kuchukua wadhifa wa spika wa bunge, wadhifa wenye nguvu kubwa ambao ni wa pili baada ya makamu wa rais katika kurithi ofisi ya rais.

McCarthy anayetokea California alishindwa katika duru ya nne, ya tano na ya sita ya uchaguzi wa kuwa spika. Alipata kura 201 pekee kati ya 218 zinazohitajika, wakati Warepublican 20 wakimpigia kura jana Mjumbe Byron Donalds, Merepublican aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2020. Mrepublican mmoja alikataa kumuunga mkono mgombea yeyote. Wademocrat wote 212 walimpigia kura Jeffries. Akizungumza wakati akimpigia McCarthy kura, Mrepublican Kat Cammack wa Florida alisema mambo kwa sasa ni magumu

Wapinzani walisema vita hivyo vya uongozi huenda vikaendelea kwa wiki kadhaa. Wabunge kisha walipiga kura na kwenda nyumbani jana jioni na kujaribu tena leo mchana.

Mkwamo huo unaibua maswali kuhusu uwezo wa Warepublican kuongoza katika miaka miwili ijayo wakati wakionekana kuyumba katika kile ambacho kimsingi huwa kura ya kawaida mwanzoni mwa vikao vya bunge.


Post a Comment

Previous Post Next Post