Mkoa wa Lindi umepokea
fedha kiasi cha shilingi Milioni 110 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi
wenye mahitaji maalum katika shule ya Msingi Mtanga Wilayani Kilwa Mkoani Lindi
Katibu Tawala Mkoa wa Lindi
Ngusa Samike akiwa katika kikao kazi cha uboreshaji wa usimamizi wa Elimu
Msingi na Sekondari Mkoani humo kilichofanyika Nyangao Januari 14,2023 amesema kiasi
hicho cha fedha ni sehemu ya mgao wa fedha za sherehe za uhuru za mwaka 2022
ambazo zilielekezwa zijenge miundombinu ya watoto wenye mahitaji maalum.
Sambamba na hayo, akizungumzia
kuhusu uandikishaji wa wanafunzi wa madarasa ya awali na darasa la kwanza kwa
mwaka 2023 amebainisha kuwa hadi sasa Mkoa wa Lindi umeandikisha kwa asilimia 85
ya maoteo.
Naye mkuu wa Wilaya ya
Lindi SHAIBU NDEMANGA amewaomba viongozi na wote wanaosimamia sekta ya elimu
kusimamia miongozo iliyowekwa kwenye sekta hiyo ili kufikia malengo.
Post a Comment