YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Kanali Ahmed Abasi.

Na Elizabeth Msagula

Licha ya kuwepo kwa mafanikio katika sekta ya elimu, inaelezwa kuwa bado kuna changamoto zinazokwamisha kufikia malengo katika uboreshaji na usimamizi wa shughuli za elimu nchini.

Changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa wanafunzi wanaomaliza darasa la kwanza bila kuwa na umahili na ustadi wa kusoma, kuandika na kuhesabu huku wengine wakiwa wanamaliza elimu ya msingi na kidato cha nne wakiwa na uwezo hafifu wa kumudu stadi za lugha  ya kingereza ingawa somo hilo hufundishwa kuanzia darasa la tatu hadi la Saba lakini Pia ni lugha ya kufundishia kwa shule za Sekondari.


Changamoto nyingine inayoelezwa ni kushuka kwa ufaulu kwa wanafunzi ambao umekuwa kwa asilimia 0.89 kwa mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 1.8 kwa mwaka 2021.

Kufuatia hayo, Ofisi ya Rais TAMISEMI imeendelea kuwaelekeza wasimamizi wote wa Elimu nchini kujipanga ili kuhakikisha wanafunzi katika ngazi zote wanapata ujuzi, stadi na maarifa unaotakiwa ikiwa ni pamoja na wanafunzi wanaomaliza darasa la kwanza  wanakuwa na umahili wa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu na wale wanaomaliza darasa la saba wawe na umahili wa kujua lugha ya kiingereza.

Hayo yameelezwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Angela Kairuki Mkoani Lindi katika kikao cha kutathimini namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa elimu msingi na sekondari Mkoani Lindi, kikao ambacho amewakilishwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Kanali Ahmed Abasi.


Naye, Mkurugenzi Msaidizi, ofisi ya Rais TAMISEMI Mwalimu Suzan Nusu amesema ili kufikia malengo kwa darasa awali,la kwanza   na la Pili waache utaratibu wa kuwaweka waalimu waliochoka kufundisha madarasa hayo.

Awali, Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ngusa Samike ameeleza kuwa, kupitia maboresho yaliyofanyika na utekelezaji wa Mpango mkakati wa elimu wa Mkoa ulioanza mwaka 2019 ,wameeleza kuwa wamepunguza kwa asilimia 99.9 tatizo la wanafunzi wasiojua Kusoma,kuandika na kuhesabu  kwenye upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kwa mwaka 2022.

Post a Comment

Previous Post Next Post