YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA kinatarajia kuzindua ajenda zaidi ya 10 zitakazokiongoza kwenye mikutano yake ya hadhara ambayo inatarajiwa kuzinduliwa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe, Januari 21, 2023 jijini Mwanza.

Uzinduzi wa ajenda hizo utafanyika sambamba na uzinduzi wa mikutano ya hadhara ya chama hicho kwenye kanda mbili ambazo ni kanda ya Ziwa Viktoria na kanda ya Serengeti.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema Mbowe na viongozi wengine wa kitaifa wa Chadema wataongoza uzinduzi wa mikutano ya hadhara sambamba na ajenda za chama.

Post a Comment

Previous Post Next Post