YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


Hussein Bashe, Waziri wa kilimo nchini Tanzania

Na Alfred Mlonganile

Waziri wa kilimo nchini Tanzania Hussein Bashe (MB) leo January 11,2023 amewashukuru wale wote walioshiriki na kuunga mkono Programe ya Vijana (BBT) kupitia ukurasa wake wa Twitter baada ya mradi huo kuanza kufanyiwa utekelezwaji. 

“Salaam, Kama mnakumbuka tulitangaza Programe ya Vijana (BBT) kwenye kilimo na Blockfarms Tunashukuru sasa implementation stage imeanza.
Nawashukuru timu yote iliyoshiriki kuanzia ideation, program design hadi implementation plan. Please share Training ,Grants na Soft loan gazette.” Ameandika Bashe.

July 23, 2022 aliweka wazi juu ya uzinduzi wa shamba la kwanza la hekari 11,453 kwajili ya Mradi wa Vijana wa Block Farm. Pia alisema kumetengwa eneo maalum kwa ajili ya kujenga makazi ya vijana watakaoshiriki kwenye shughuli za kilimo pamoja na ujenzi wa eneo maalum la malisho, maji na majosho ya mifugo.

Aidha Aug. 7,2022 alitoa mrejesho wa kinachoendela katika mradi huo katika kuyafikia malengo ya Ajenda 10/30

Awali Waziri Bashe aliuliza swali kupitia ukurasa wake wa Twitter Septemba 7,2022 lililokuwa na lengo la kuwataka wananchi kutoa mawazo yao kuhusu kilimo na usalama wa chakula kwa nchi za Afrika haswa nchiniTanzania

“Ukiwa na muda tafadhali nipe mawazo yako kuhusu Kilimo na usalama wa Chakula kwa nchi za Afrika haswa hapa nyumbani kwetu Tanzania. Nini kifanyike? Nini kiboreshwe?” Aliandika Bashe

Post a Comment

Previous Post Next Post