YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akizungumza na viongozi mbalimbali alipotembelea eneo la mradi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndaki ya Kilimo Wilayani Runagwa Mkoa wa Lindi

Na Elizabeth Msagula

Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa imetakiwa kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa hati ya eneo la Kitandi kitakapojengwa chuo cha Dar es Salaam ndaki ya Kilimo na kukabidhi kwa chuo hicho ili taratibu za ujenzi ziweze kuanza.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Jakaya mrisho Kikwete alipotembelea kuona maeneo ambayo yatajengwa matawi ya chuo hicho ikiwemo eneo la Ngongo Manispaa ya Lindi na Kitandi Wilayani Ruangwa eneo lenye ukubwa wa Ekari 405 ambapo watu watasoma katika ndaki hiyo kwa shahada ya  pili na ya tatu.

Mkuu huyo wa Chuo Dkt. Kikwete ametaka kumalizwa kwa migogoro yote ya ardhi kwenye maeneo hayo na taratibu zingine kama fidia kwa wananchi ili ujenzi uanze mwezi June 2023.

Eneo la Kitandi kitakapojengwa chuo cha Dar es Salaam ndaki ya Kilimo

Kwa upande wake Afisa Ardhi wa halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Peter Hanjai amesema kwa sasa wanasubiri ripoti ya mtathmini na halmashauri iendelee na taratibu zingine za utoaji wa hati ambapo Pamoja na hayo ameahidi kabla ya kufikia mwezi Juni hati hiyo itakuwa imepatikana.

Post a Comment

Previous Post Next Post