Happy Mremi - Morogoro

Zaidi ya shilingi bilioni 66 imepitishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020-2021 katika halmashauri wilaya ya Kilosa ambapo bajeti hiyo imejikita katika kumkomboa mkulima, kuboresha afya ya mama na mtoto, pamoja na elimu hii ni katika kufikia malengo ya serikali ya kuinua uchumi wa taifa na mtu mmoja mmoja

Akiwa katika kikao maalum cha kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha katika halmashauri hiyo mkurugenzi mtendaji wa wilaya Kilosa Asajile Mwambambale ameeleza vyanzo vya mapato yatakayofanikisha bajeti hiyo.

Aidha mbunge wa jimbo Mikumi Denis Londo amesema kuwa bajeti hiyo itakuwa chachu   ya kuongeza maendeleo katika wilaya hiyo kwa kutekeleza mipango mikakati waliyojiwekea, huku baadhi ya madiwani kutoka katika wilaya ya kilosa wakaeleza ni kwa namna gani bajeti hiyo iliyopitishwa itakavyowasaidia wananchi katika kutoa huduma za kijamii kwenye kata zao.

 



 

Post a Comment

Previous Post Next Post