YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

 
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameagiza kukamatwa kwa Mkandarasi na Mshauri Muelekezi wa Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupooza umeme cha Kilombero Mkoani Morogoro endapo ujenzi hautaanza ndani ya siku kumi alizozitoa
 
Na Happy Mremi - Morogoro 

Moja ya sekta muhimu hapa nchini ni sekta ya nishati,serikali imewekeza nguvu kubwa katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya nishati ya umeme ili kuboresha shughuli mbalimbali za kiuchumi hapa nchini kwani kuwepo kwa umeme wa uhakika kwa wananchi, viwanda,na katika taasisi mbalimbali  ni kipaumbele mojawapo cha serikali

Serikali imeamua kujenga kituo cha kupooza umeme wilayani Kilombero ili kupunguza changamoto ya ukatikaji umeme katika wilaya hiyo.

Mivutano baina ya wataalamu yaani mkandarasi na msimamizi muelekezi  wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme kitakachoigharimu serikali zaidi ya bilioni 20 kunamfikisha waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani wilayani humo mkoani Morogoro na kusikiliza chanzo cha mgogoro unaopelekea ujenzi huo kutoanza kwa wakati  na kuagiza ujenzi uanze ndani ya siku kumi kutokana na ujenzi huo kucheleweshwa kwa takribani mwaka mmoja.

Kukamilika kwa kituo hicho  kutaondoa changamoto ya  kukatika kwa umeme katika wilaya za kilombero,malinyi  na ulanga mkoani Morogoro kwani kituo kitakua na uwezo kuingiza na kupooza umeme voltage 220 na kutoa voltage 33 kwa wananchi.

 


 
 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post