YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


Ili kuwa na Jamii imara yenye demokrasia na haki, ni muhimu kuwa na vyombo vya habari kwa maana ya televisheni, redio na magazeti pamoja na mitandao ya kijamii katika utekelezwaji wa haki ya kujieleza, kutoa taarifa na kupata taarifa.

Tasnia ya habari nchini Tanzania inakabiliwa na changamoto nyingi zinazoathiri moja kwa moja dhima yake ya kuendeleza demokrasia, utawala bora na uwajibikaji. A wali ya yote, miaka mitatu iliyopita, Tanzania imetunga sheria kadhaa zinazozuia uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza na zinazokazia ukali wa sheria zilizopo ambazo ni vikwazo katika kuhabarisha wananchi.


Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye vyombo vingi vya habari Afrika Mashariki. Hata hivyo vyombo vingi kati ya hivyo ni vidogo, havina rasilimali za kutosha, dhaifu na ambavyo waandishi wake wa habari hukutana na changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ya kitaaluma na katika kuhakikisha kwamba wanatoa habari zenye uyakinifu.

Vipengele mojawapo katika changamoto za vyombo vya habari ni pamoja na mitaala ya Elimu kutokidhi mahitaji ya soko, ambapo wanahabari wanafunzi wanakosa ujuzi katika kutekeleza majukumu yao ya kitaaluma na katika kuhakikisha kwamba wanatoa habari zenye uyakinifu.

TAZAMA MAKALA HII KWA KUFUATA LINK HAPA CHINI:




 

Mawasiliano:
Mobile: +255 688 94 2017
Email:   mr.mlonganile@gmail.com

Post a Comment

Previous Post Next Post