Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amewatoa hofu watanzania na kuwahahikikishia kuwa mradi wa umeme wa mwalimu Nyerere ulioko kati ya Rufiji na mkoa wa Morogoro utakamilika kwa wakati na utakua na gharama nafuu.

 


Akiwa katika ziara ya siku moja ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi huo Waziri Mkuu Majaliwa ameonyesha kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi ambapo amesema kuwa maeneo muhimu ya mradi huo yamefika asilimia 47 ya ujenzi huku akieleza kuwa mradi utakamilika ifikapo Juni mwakani kama ilivyopangwa na kuwa umeme unaozalishwa kwa maji utakua wa bei nafuu zaidi.

Aidha Waziri Mkuu amemtaka naibu waziri wa nishati kusimamia mradi huo kwa ukaribu zaidi na kuongeza kuwa ni vizuri wananchi walioko karibu wakipewa fursa ya kutembelea mradi huo ili kuepuka maneno ya wapotoshaji.

Post a Comment

Previous Post Next Post