Wadau wa ushirika Mkoani Lindi ikiwemo mitandao ya simu wamehimizwa kushirikiana na wakulima kwa kutoa huduma bora zitakazowafanya kuendelea kupitishia malipo ya mazao kupitia mitandao yao.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bi. Zainab Telack amehimiza hayo Mei 18, 2025 alipotembelea banda  la kampuni ya Simu ya Yas ambayo kipekee inatoa fursa kwa wakulima kulipwa pesa wanazopata baada ya kuuza mazao yao.

Haya yamejiri katika Kilele cha Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoani humo lililofanyika kwa siku mbili kuanzia Mei 17 hadi 18, 2025 Mjini Lindi.

Post a Comment

Previous Post Next Post