Mkoa wa Lindi umenufaika kwa ujio wa Madaktari bingwa wabobevu 47 kwa kada mbalimbali ambao wataenda katika halmashauri zote za mkoa huo kukamilisha zoezi litakalodumu kwa muda wa siku 6 kupitia kampeni ya Mama Samia awamu ya tatu.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary aliyeeleza kuwa, madaktari bingwa wabobevu hao utakwenda kutatua changamoto kwa wananchi, hivyo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwenye hospitali zote za wilaya na amewataka waganga wakuu wa wilaya kuweka mazingira wezeshi ili shughuli hizo zisikwame.

Kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa msafara wa madaktari bingwa wabobevu Daktari Michael Mbele, kila halmashauri  itapata madaktari 7 ambao wamebobea kwenye kada za upasuaji, magonjwa ya wototo, mfumo wa pua koo na masikio, magonjwa ya watoto na akina mama pamoja  na uzazi.

Ameongeza kuwa, Licha ya kuwatibu wagonjwa, watatoa mafunzo kwa madaktari wengine kutoka kwenye vituo husika kwa hospitali za halmashauri zote. Hivyo wameomba ushirikiano kutoka kwao ili zoezi hili limalizike kama ilivyopangwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post