Ikiwa imepita Siku moja tangu Rais Joe Biden atangazwe kupata maambukizi ya COVID-19 na kusitisha kampeni, Vyombo mbalimbali vya Habari vya Kimataifa vimeripoti Rais Mstaafu, Barack Obama na Spika Mstaafu, Nancy Pelosi wamemshauri kiongozi huyo kutafakari upya juu ya kushindana na Donald Trump


Licha ya kauli ya Biden ya hivi karibuni kuwa hawezi kujiondoa katika mchakato wa kuwania Urais kwa Awamu ya Pili, inadaiwa hali yake ya kiafya na uwezekano wa kushindana na Rais wa zamani, Trump unazidi kuwapa wasiwasi Makada na Wadhamini wa Democrats 

Inaelezwa kitendo cha Biden kushindwa kukabiliana vizuri na Trump katika Mdahalo, kuchanganya majina kwa kumfananisha Makamu wake na Trump, kumtambulisha Rais wa Ukraine kama Putin ni baadhi ya mambo yanayochangia kuonesha uimara wa Afya ya Rais uko shakani

Post a Comment

Previous Post Next Post