Mahakama ya Rufaa ya Tanzania mkoani Arusha, chini ya Majaji watatu Omar Othman Makungu, Stella Mugasha na Dkt. Mary Levira imemuchia huru mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Abubakar Shaban, baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la ulawiti.

Shabani alihukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya hakimu mkazi Arusha  baada ya kujiridhisha kuwa, tarehe 24 Januari, 2018 katika eneo la  Sanawari, Mkoani Arusha, alimwingilia kinyume na maumbile mvulana wa  miaka 2 na nusu (jina limehifadhiwa kulinda utambulisho). Kwa wakati huo  wa hukumu Shaban alikua na umri wa miaka kumi na nane


Post a Comment

Previous Post Next Post