Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amekutana na wakala wa ndani anaehusika na usimamizi wa fedha za Global fund ukiongozwa na Sarah Bisanda na Cletus Kiyuga na kujadili maeneo ya ushirikiano ili kuleta ufanisi na tija katika miradi inayofadhiliwa na Global Fund


Kikao hicho kimefanyika leo, Julai 19, 2024 jijini Dodoma, ambapo Wizara ya Afya pamoja na LFA imejadili juu ya kuendelea kushirikiana katika nyanja mbali mbali ili kuendelea kutekeleza afua za kutokomeza magonjwa yanayofadhiliwa na Global Fund ifikapo mwaka 2030.

Aidha Katibu Mkuu Dkt. John Jingu amewataka LFA kuwajengea uwezo wa kitaalamu watumishi wa wizara Pamoja na wa miradi misonge inayofadhiliwa na Global Fund ili kufikia malengo ya kutokomeza magonjwa hayo ifikapo mwaka 2030

Post a Comment

Previous Post Next Post