YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Mtoto Said Mohamed (12) mwanafunzi wa shule ya msingi Somanga_Simu amefariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki maarufu bodaboda alipokuwa anavuka barabara majira ya saa tano asubuhi karibu nae neo la shule.


Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza na Mashujaa FM wamesema dereva huyo wa bodaboda alikuwa katika mwendo mkali hali iliyopelekea kumgonga mwanafunzi huyo.

Mganga mfawidhi wa kituo Cha afya Tingi wilayani Kilwa mkoani Lindi Dr. Alfred Chinyeu amesema marehemu huyo mpaka anafikishwa katika kituo hicho cha afya alikuwa amefariki huku uchunguzi ukionesha majeraha katika maeneo ya kichwa.

Hata hivyo Mashujaa FM imezungumza na kamanda WA Polisi mkoani humo ACP  Pili Mande ambaye amesema haajafikiwa na taarifa hiyo na ameahidi kufuatilia zaidi tukio hilo. 

Post a Comment

Previous Post Next Post