YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndugu Mohamed Ali Kawaida (MCC) akizungumza na waandishi wa habari kuonesha msimamo wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM ya kuunga mkono hoja ya Uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam.


Mkutano huo umefanyika kwenye Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya UVCCM Upanga Jijini Dar es Salaam 15 Julai, 2023.

Aidha Ndg, Kawaida, amesisitiza kuwepo kwa Maandamano ya Amani ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha, kuendesha na kuendeleza maeneo ya Bandari nchini. Maandamano hayo yatafanyika nchi nzima ambapo yatazinduliwa rasmi Mkoani Dar es Salaam siku ya tarehe 18 Julai, 2023.

Credit: Millardayo

Post a Comment

Previous Post Next Post