YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto UNICEF linasema mzozo wa Sudan umepelekea zaidi ya watoto milioni moja kuachwa bila makao.

Picha ya maktaba, Sudan

UNICEF inasema kati ya hao 1,270,000 wanatokea jimbo la Darfur. Katika taarifa, shirika hilo kupitia mwakilishi wake nchini Sudan, Mandeep O'Brien, limesema takriban watoto 330 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 1,900 kujeruhiwa.  

O'brien ameongeza kwamba inakadiriwa kuwa watoto milioni 13 wanahitaji misaada ya kiutu. Mapigano yameshuhudiwa nchini Sudan tangu katikati ya mwezi Aprili kati ya vikosi vya mkuu wa jeshi la nchi hiyo Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo.

Post a Comment

Previous Post Next Post