YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Baadhi ya wasomi, wazazi na wadau wa elimu nchini wameeleza mtazamo wao kuhusu wimbi la sasa la wahitimu wengi wa kidato cha nne, kuachana na masomo ya kidato cha tano na kutimkia vyuo vya kati kusomea fani mbalimbali.  

Picha ya Maktaba

Akizungumzia wimbi hilo, Mkufunzi na Ofisa Uhusiano wa Taasisi ya Maendeleo ya Jamii ya TICD-Tengeru, Adrian Lyapembile, alisema wanafunzi wengi wanafanya hivyo kwa kuwa wanaona vyuo vya kati vitawasogeza haraka kupata ujuzi na ajira, badala ya kupoteza muda wa miaka miwili sekondari, na wakihitimu watalazimika kusoma tena diploma miaka miwili.  

“Wazazi wengi na hata wanafunzi wenyewe wanaamini shule ile ya miaka miwili ya kidato cha tano na cha sita ni kama wanakwenda kupoteza muda, kwa sababu ile miaka miwili akimaliza anarudi bila ujuzi wowote.  

“Kwa hiyo, wengi wanapendelea mtoto aende vyuo vya kati, akasomee ujuzi ambao atarudi nao na utamsaidia kupata ajira au kujiari mwenyewe. Ndiyo! miaka miwili atakuwa amesoma NTA Level 4 na NTA Level 5, ambayo ni ngazi ya cheti na akiongeza mwaka wa tatu anapata Diploma.  

“Inaonekana ni rahisi zaidi kwa sababu huyo aliyesoma kidato cha tano na sita, bado atahitaji tena kusoma miaka miwili ya kupata diploma,” alifafanua.

1 Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post