YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Watu wanne akiwemo mwanamke mmoja na watoto wake watatu wakazi katika kijiji cha Chidede Kata ya Luagala wilayani Tandahimba mkoani Mtwara, wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuungua moto usiku wa Juni 21  Moja ya shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la Saidi Hassan amesema tukio hilo limetokea saa 4 usiku wa kuamkia Juni 21, 2023 kwa nyumba ya, Rehema Nyapala kuungua moto na kusababisha vifo vya watoto watatu kufariki dunia papo hapo huku mmiliki wa nyumba hiyo akiokolewa kutoka ndani.  

Picha ya Maktaba

Saidi amesema yeye alikuwa anatokea katika banda la video baada ya mmoja wao walikuwa katika banda hilo kutoka nje na kuona nyumba ikiungua moto na kutoa taarifa kwa watu wote waliokuwemo katika banda hilo.  

Saidi ameongeza kwa kusema kuwa, baada ya watu wa karibu kubomoa mlango, alifika Khadija Mshamu Likundende ambaye alimtoa, Rehema Nyapala akiwa ameungua vibaya na moto katika mwili wake na kumtoa nje huku watoto wakishindwa kuwaokoa kwa sababu moto kuwa mkali na walikuwa tayari wamepoteza maisha wakiwa katika vitanda vyao.  

Baada ya Rehema Nyapala kuokolewa alikimbizwa kituo cha afya Luagala ambapo nao walimpa rufaa kwenda hospitali ya Nyangao na asubuhi ya leo Juni 22,2023 walipokea taarifa kuwa, Rehema Nyapala amefarikia dunia.  

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema amesema kuwa Juni 21 saa nne usiku katika kijiji cha Chidede Rehema Hamisi (40) mkazi wa kijiji hicho akiwa ammelala nyumbani kwake na wanae wawili ambao ni Adhiru Shaha Bakari (12) mwafunzi wa darasa la tatu Shule ya Msingi Chidede, Imran Shadhili (3) na Muba Jafari Salum (15) ambaye ni mtoto wa dada yake, wakiwa wamelala usiku, nyumba yao ilishika moto na kuuungua na kusababisha vifo vya watu watatu katika eneo hilo la tukio.

Post a Comment

Previous Post Next Post