YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu imetoa agizo hilo ikiwa ni Siku moja tangu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, kuitaka Serikali kuwawajibisha Waajiri wanaoshindwa kuwasilisha Michango pamoja na Mifuko kutolipa madeni ya Wanachama wake.

Prof. Joyce Ndalichako, Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu

Wizara imeagiza Majina ya Waajiri wote Sugu wasiowasilisha na wanaodaiwa Michango ya Wafanyakazi kupelekwa kwa Mameneja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wa Mikoa ndani ya siku 7 kuanzia leo Juni 22, 2023.

Aidha, imeitaka Mifuko yote kukamilisha zoezi la kusaini Mikataba ya kulipa madeni yote ya michango ya wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kabla ya Juni 30, 2023.

Post a Comment

Previous Post Next Post