YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Eliezer Mbuki Feleshi

“Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna,”

“Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?” Alihoji Jaji Feleshi.

“Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?”

“Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi,” alisisitiza.

“Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika,” 

“Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari),” 

Post a Comment

Previous Post Next Post