YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Ujerumani na Afrika Kusini zinakusudia kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika nyanya tofauti licha ya kuwa na misimamo inayotofautiana kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Afrika Kusini.


Waziri Annalena Baerbock, amefanya mazungumnzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Afrika Kusini Naledi Pandor na kwa pamoja wamesisitiza umuhimu wa uhusiano baina ya nchi hizo mbili walipokutana katika mji mkuu wa Pretoria. Ajenda zilizojitokeza ni pamoja na kuimarisha ushirikiano katika masuala ya uchumi, utalii, mapambano dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi na janga la Covid-19. 

Suala la vita vya Urusi nchini Ukraine, pia lilitawala mazungumzo ya mawaziri hao wawili, huku waziri Baerbock akiitaka Urusi "kuacha kuishambulia" Ukraine katika mazungumzo yake na Pandor wakati wa ziara yake ya siku moja mjini Pretoria.Ujerumani na Afrika Kusini zaazimia kuimarisha ushirikiano wao licha ya kuwa na maoni tofauti katika kukabiliana na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. 

Kuhusu tukio la uasi la mwishoni mwa juma lililofanywa na kundi la mamluki la Wagner, waziri Baerbock amewaeleza waandishi wa habari kwamba Ujerumani "haiingilii kati" kile alichokitaja kuwa "masuala ya Urusi", lakini akatahadharisha kwamba Ujerumani "inafuatilia kwa karibu" hali ya mambo ingawa msukumo wao unasalia kuwa vita vya Ukraine. 

"Na hali ilivyokuwa mwishoni mwa juma lililopita inadhihirisha kwa mara nyingine tena kwamba Putin pia anahatarisha usalama wa nchi yake kwa vita hivi ambavyo ni kinyume na sheria za kimataifa, na ndiyo maana wito wetu wa dharura ni kwamba vita hivi lazima viishe. Hilo liko mikononi mwa Rais wa Urusi. Sote duniani tunatamani amani. Na ndio maana amani ndio jambo muhimu zaidi kwetu," alisema waziri Baerbock.


Credit: DW

Post a Comment

Previous Post Next Post