YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Mwanamke anayeitwa Salma Shaibu(28) amefariki dunia Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi baada ya kujiua kwa kunywa sumu ya kuulia wadudu chanzo kikidaiwa ni kujihisi mwenye hatia baada ya kukiri mwenyewe kabla ya kujiua ya kuwa alichepuka na Mwanaume mwingine.  

Picha ya Mkataba

Salma ambaye ameacha Watoto wawili akiwemo mkubwa ambaye anasoma elimu ya awali, enzi za uhai wake alikuwa akiishi na Mumewe Ramadhan Hamisi Wilayani Masasi Mkoani Mtwara na akasafiri kwenda Wilayani Newala, Mtwara ambako alishawishika na kuingia kwenye mahusiano na Mwanaume mwingine, na baada ya kurudi nyumbani kwa Mumewe Masasi, Salma hakuwa mwenye furaha kwakuwa nafsi ilikuwa inamsuta.  

Salma aliamua kumsimulia Rafiki yake wa kike na Mdogo wake na wote walimpa moyo na kumwambia akae kimya kwani jambo hilo akilisikia Mumewe linaweza kuzua balaa lakini aliendelea kuonekana mwenye simanzi mpaka Mumewe akahisi tofauti na kuumuliza Rafiki wa Mkewe ambapo alimsimulia kila kitu lakini Mume huyo hakukasirika na alisema ni jambo la kawaida na akamwambia Mkewe asiwe na wasiwasi.  

Licha ya kusamehewa na Mumewe Salma hakuwa na amani na akaaga kwenda Wilayani Nachingwea kumsalimia Baba yake aliyekuwa mgonjwa ambako alikaa siku mbili na kuamua kunywa sumu kali ya kuulia wadudu kwenye mikorosho na kuacha na karatasi yenye ujumbe unaosema “NIMESHINDWA KUISHI KWA MAKOSA YANGU MWENYEWE” huku mkononi mwake akiwa ameandika ujumbe ambao unaendana sawa na maneno aliyoyaandika kwenye karatasi na kusisitiza sio tatizo la yeyote bali ni ujinga wake na kujihisi ameikosea Familia na Mungu wake.  

Baada ya Mwili wa Marehemu kufikishwa kwenye Hospitali ya Mnero, imebainika ya kuwa alifariki baada ya sumu aliyokunywa kuathiri zaidi viungo vya ndani ya mwili na mfumo wa upumuaji, RPC wa Lindi Pili Mande, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa vijana kushirikisha Watu mbalimbali masuala yanayowasibu na kupata ushauri namna ya kutatua huku akiwaelekeza kutumia dawati la jinsia la Jeshi hilo kuelezea changamoto mbalimbali za kisaikolojia na mahusiano ili kupata msaada na kuepusha maamuzi magumu ya kujiua.

Post a Comment

Previous Post Next Post