YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW

Wizara ya uwekezaji viwanda na biashara kupitia mkakati unaolenga kutatua matatizo na changamoto za uendeshaji wa biashara (KAIZEN) kupitia uvumbuzi wa mawazo, maarifa na ushiriki wa watumishi imetoa mafunzo kwa wamiliki wa viwanda vidogo na vikubwa mkoani Lindi ikiwa ni mkoa wa 16 kufikiwa na mchakato huo kati ya mikoa 31 nchini.


Akizungumza na waandishi wa Habari kaimu mmurugenzi mkuu wa KAIZEN, Richard Kuleza, amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea wafanyabiashara uelewa wa pamoja ili kuweza kuongeza Tija na ubora Katika uzalishaji mali na kukua kiuchumi.


Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Dk. Bora Haule Amesema mafunzo hayo yamekuja muda sahihi na amewapongeza Wizara ya uwekezaji, viwanda na biashara kwa kuwafikia wafanyabiashara Lindi kwani mkoa wa Lindi Unaenda kutekeleza miradi mikubwa hivyo mafunzo hayo yataleta Tija.


Pia Dk. Bora ametoa wito na amewakaribisha wawezekaji kuja katika mkoa wa Lindi kwa wingi na kutoa mafunzo kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea wadau wa maendeleo na wafanyabiashara mkoani Lindi kuingia katika soko la ushindani.

Post a Comment

Previous Post Next Post