Matumizi ya mifumo ya Tehama katika utunzaji wa kumbukumbu ni miongoni mwa vipaumbele saba vya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika bajeti yake ya mwaka 2023/24. Hayo yalielezwa jana na Waziri wa wizara hiyo, Dk Angelina Mabula, akitaja pia utoaji huduma, upatikanaji wa taarifa za ardhi na kuweka mazingira rafiki ya upatikanaji ardhi ya uwekezaji kama vipaumbele vingine. 

Waziri wa wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk Angelina Mabula

Pia amezungumzia kuimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro ya ardhi, kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi, kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali yatokanayo na sekta ya ardhi, ikiwa na matumizi ya teknolojia pamoja na kuimarisha mipaka ya kimataifa. 

Waziri Mabula alisema Serikali imejizatiti katika kuhakikisha inamaliza migogoro ya ardhi katika maeneo mengi na jambo hilo litafanikiwa kutokana na mikakati ndani ya wizara na Serikali. 

Dk Mabula ameomba Bunge liidhinishe Shilingi bilioni 171.372  ikiwa ni ongezeko la Shilingi bilioni 8.2 ya bajeti ya mwaka jana ambayo ilikuwa Sh 163.166 bilioni, kwa ajili ya matumizi ya wizara hiyo na taasisi zake.

Post a Comment

Previous Post Next Post