Yusra Hassan Ally binti mwenye umri wa miaka 11 kutoka kata ya Nyengedi halmashauri ya Mtama mkoani Lindi, ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga siku ya tarehe 17 May, 2023 saa nane mchana huku chanzo cha kifo hicho kikiwa bado hakijajulikana.

Picha ya Maktaba

Akizungumza kwa njia ya simu, mwenyekiti wa kijiji cha Nyegedi A Omari Baisa anasimulia kuwa, marehemu alikuwa akiishi na bibi yake mzaa baba baada ya wazazi wake kutengana.

Kamishna msaidizi wa Polisi Alhaji Kabaleke Salim Hassan ambaye ni Afisa Mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa Lindi na sasa ni kaimu kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Lindi anathibitisha kutokea kwa tukio hilo na baada ya upelelezi ikiwemo kuwahoji watu mbalimbali Pamoja na walezi wa marehemu YUSRA hawajafanikiwa kujua chanzo cha tukio hilo.

Kamishna msaidizi wa Polisi Alhaji Kabaleke Salim Hassan ambaye ni Afisa Mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa Lindi

Katika tukio jingine, mwanamama aliyehamika kwa jina Somoe Said (65) mkazi wa Kijiji cha Nachui hukohuko Nyengedi tarehe 24 May, 2023 saa 11 jioni alivamiwa na Mamba alipokwenda kuoga katika mto Lukuledi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi, Somoe alipatikana siku ya tatu baada ya kufanyika msako kwa kushirikiana na askari wa maliasili huku mwili wake ukiwa umeliwa na Mamba huyo na kusalia sehemu ya Kichwa.

Afisa Mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa Lindi, Kamishna msaidizi wa Polisi Alhaji Kabaleke, ametoa tahadhali kwa wakazi wanaoishi na kufanya shughuli zao karibu na mto Lukuledi na kuwaomba kushirikiana na watu wa maliasili ili kutambua maeneo hatarishi kama vile makazi ya Mamba ambapo itasaidia kupunguza adha zinazojitokeza ikiwemo vifo.

Post a Comment

Previous Post Next Post