YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuwakilisha Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe aliyezikwa leo kijijini kwao Rondo Chiponda. 



Akiwasilisha salamu za Rais Samia waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itayaenzi yale mema ambayo Membe aliyafanya ndani ya serikali na kuwaomba watanzani kujifunza kuwa wapole na wanyenyekevu kama Membe alivyofanya enzi za uhai wake. Aidha ametaka watanzania kuishi kwa upendo na mshikamano na na moyo wa kusamehe.


Awali Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimuelezea marehemu Membe, amesema kuwa walifahamiana tangu mwaka 1984 na kuanza kufanya kazi kwa upendo mkubwa na uaminifu na kwamba kutokana na kifo chake Taifa limepoteza mwanasiasa mahiri, kasiri, mzalendo na aliyependa kusaidia watu mbalimbali. 

Pamoja na viongozi wengine, Naibu waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki balozi Nasor Mbarouk akisema Watayaishi kwa vitendo yale mema aliyowaachia.

Post a Comment

Previous Post Next Post