Serikali inatarajia kupeleka Bungeni Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Ndoa hivi karibuni ili kuamua umri sahihi wa watoto wa kike kuingia kwenye ndoa.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro (Aliyesimama)

Hayo yamebainika leo Aprili 18, 2023 bungeni jijini Dodoma wakati Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Dkt. Thea Antara aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuamua juu ya wasichana kuolewa chini ya Mika 18.

Naibu Waziri Mwanaidi amesema Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeshakusanya maoni kutoka kwa Wadau kuhusu upi umri sahihi wa kuoa au kuolewa.

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro akijibu swali la nyongeza amesema tayari maoni ya Wadau yamepokusanywa na kuchambuliwa, hatua inayofuata ni muswada kuwasiliswa Bungeni kwa ajili majadiliano ya kurekebisha sheria hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post