Kutokana na masuala ya ukatili wa watoto na wanawake kukithiri, athari inayosababisha kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili sambamba na matukio ya ulawiti na Ushoga, jeshi la Polisi Mkoani Lindi kupitia Dawati la Jinsia na watoto, limetoa elimu kwa wazazi na walezi wa kikristo kutoka kanisa la kilutheri mkoani Lindi.


Na Humphrey Moris

Elimu hiyo imetolewa kwa dhumuni la kumlinda mtoto, mwanamke na kupinga masuala yote ya ukatili huku wazazi wakielimishwa athari ya matukio hayo na kuongezewa ufahamu ni mambo gani hayafai kwa mtoto mdogo ili aweze kuwa salama katika makuzi yake.


Akizungumza na waumini hao, Mratibu wa dawati la Jinsia na watoto Afisa wa jeshi la Polisi,  Joyce Kitesho ametoa elimu kitaalamu kwa kuzingatia kanuni na taratibu za katiba ya Tanzania huku akihusianisha na maandiko matakatifu yanavyomsisitiza mzazi/mlezi/wanandoa kuwa walinzi na wasimamizi wa maadili kwa mtoto, huku athari ya dhambi inavyochagiza mtenda kuwa mtuhumiwa kutokana na kanuni za sheria.

Post a Comment

Previous Post Next Post