Wakala wa vipimo mkoa wa Lindi wametoa siku 14 kwa wauzaji wa gesi za kupikia mkoa wa Lindi kuhakikisha wanakuwa na mizani kwa ajili ya kupima gesi pindi wateja wanapokwenda kununua bidhaa hiyo.


Agizo hilo limetolewa na meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa Lindi Andrew Mbwambo wakati wa kikao baina ya wakala wa vipimo na wauzaji wa gesi za kupikia kilichofanyika kwenye ofisi za wakala huyo ambapo amesema kila muuza gesi ahakikishe ana mzani uliohakikiwa.

Sambamba na hilo amebainisha kwamba baada ya siku 14, wauzaji ambao hawatakuwa na mizani kwenye maeneo yao, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na amewataka wauzaji hao wa gesi kuhakikisha wanakidhi vigezo kwa sababu kuna wauzaji wengine wana matawi zaidi ya moja ya uuzaji wa gesi za kupikia lakini hawana vigezo.

Nao baadhi ya wauzaji wa gesi za kupikia waliohudhuria kikao hicho wameshukuru kupata elimu inayohusu umuhimu wa mizani ambayo wamesema itawasaidia kuwasiliana vizuri na wateja wao, huku wakiwasihi wateja wanapokwenda kununua gesi wahakikishe wanapimiwa na mzani uliohakikiwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post