Wakandarasi wawili wazawa, STC Construction Company Limited na Emirate Builders Co. Limited wanaotekeleza mradi mkubwa wa maji wa Nyangao - Ruangwa - Nachingwea leo Machi 1, 2023 wamekabidhiwa rasmi eneo patakapojengwa mradi huo ambapo ni Jirani na chanzo cha mto Nyangao na Chiuwe Wilaya ya Lindi. 


Mradi huo, unajumuisha vijiji 34 vilivyopo Wilaya ya Ruangwa, vijiji 21 kutoka wilaya ya Nachingwea na Kijiji kimoja kutoka wilaya ya Lindi vyenye wakazi wanaokadiliwa kufikia 128,657 na hivyo kuwezesha kufikia lengo la kitaifa la upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kwa zaidi ya asilimia 85.

Kwa upande wa wakandarasi hao, wameomba kupewa ushirikiano katika Wilaya zote ambazo mradi unapita na kuahidi kutekeleza kwa uaminifu mkubwa na kwa wakati ili kutoa matumaini kwa serikali na wananchi kuwa, wakandarasi wa ndani wanao uwezo wa kutekeleza majukumu kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Lindi ametumia nafasi hiyo kuwasisitiza kukamilisha mradi huo bila ya kuwa na visingizio ikiwemo mvua.

Mkataba wa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Nyangao – Ruangwa – Nachingwea ulisainiwa Februari 18, 2023 katika Kijiji cha Nandagara Wilayani Ruangwa, kati ya wakandarasi hao na Wizara ya Maji kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Post a Comment

Previous Post Next Post