Wakati dunia ikiadhimisha siku ya wanawake Duniani, wanawake wa kata ya Rutamba halmashauri ya manispaa ya Lindi wamelia na changamoto ya uchakavu wa miundombinu katika kituo cha afya cha Rutamba.


Jengo la kutunzia maiti (Mochwari) kituo cha afya cha Rutamba Manispaa ya Lindi

Wamelalamikia hayo baada ya wanawake kutoka Mashujaa FM kufika kituoni hapo kuadhimisha siku ya wanawake ambapo miongoni mwa changamoto walizozitaja ni Pamoja na kukosekana kwa jengo la kuhifadhia maiti hali waliyoeleza kuwa ikitokea mgonjwa amefariki mwili wake hukaa wodini na wagonjwa wengine mpaka ndugu waufate mwili huo.


Aidha wamesema changamoto nyingine ni kukosekana kwa wodi ya kujifungua wajawazito hali inayowalazimu baada ya kujifungua kutumia choo kimoja na wagonjwa wananchi wengine ambao hufika hapo kupatiwa huduma mbalimbali.

Jengo la Choo Kinachotumika na wagonjwa kituo cha afya cha Rutamba

Katika hatua nyingine wameeleza kuwa Pamoja na kuwa na umeme ila inapotokea umekatika muuguzi hulazima kuomba watu wamuwashie tochi ya simu ili kumzalisha mama mjamzito hasa nyakati za usiku kwani hata solaa iliyonunuliwa na wauguzi kupitia pesa zao binafsi imeharibika. 

Wafanyakazi wanawake wakizungumza na mganga mfawidhi kituo cha afya cha Rutamba, Anton Chinguwile

Kituo hicho cha afya kimejengwa mwaka 1967 na kwa sasa kinahudumia wananchi Zaidi ya 500 kutoka katika vijiji Zaidi ya 8 na kukiwa na wataalmu 9 pekee.

Taarifa zaidi kuhusu hali ya huduma na mkakati wa serikali katika kupambana na hili zitakujia punde huku juhudi zikiendelea katika kuwasiliana na viongozi mbalimbali.

Post a Comment

Previous Post Next Post