Serikali Mkoani Lindi imewataka wadau na wataalam wa masuala ya uvuvi Mkoani humo kuwasaidia wavuvi kuwaelekeza namna bora na kuvua kwa tija na kupata nyenzo nzuri za kutumia ili kupata samaki wengi na kuvua kibiashara jambo litakalosaidia kukuza kipato cha mvuvi mmoja mmoja, halmashauri na Mkoa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack

Na Elizabeth Msagula

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack ameyasema hayo Februari 1, 2023 katika Mkutano wa wadau wa uvuvi Mkoani Lindi uliofanyika Wilayani Kilwa wenye lengo la kujadili maendeleo ya uvuvi, kuimarisha na kukuza uchumi wa bluu.
 
Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi Telack amesema licha ya mkoa huo kuwa na eneo kubwa linalofaa kwa uvuvi wa samaki takribani km 285 na mahitaji kuwa ni makubwa, bado uzalishaji wa samaki umekuwa mdogo ambapo zaidi ya kilo Milioni 1 za samaki zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 8 zimevuliwa kwa mwaka 2020/21 na kilo zaidi ya Milio 1 zenye thamani ya zaidi ya Bili 5 zimevuliwa kwa mwaka 2021/22 mkoani humo.

Akitoa taarifa ya hali ya uvuvi Mkoa wa Lindi Afisa uvuvi Mkoa wa Lindi Jumbe Kawambwa amesema malengo ya mkoa huo ni kuhakikisha wavuvi na wakuzaji wa viumbe maji wote wanakuwa katika vikundi kisha kuunganishwa na vyombo vya fedha ili waweze kutunisha mitaji yao na kupata ushauri kutoka kwa wadau wa sekta hiyo juu ya namna bora ya kupata zana bora za uvuvi na hatimaye kuongeza idadi ya vyombo vya uvuvi kutoka 2435 vya sasa hadi kufikia 5000.





Post a Comment

Previous Post Next Post