Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amechapicha maneno yenye kutia hamasa katika ukurasa wake wa Twitter kwa timu za Simba na Yanga zinazozoshiriki mashindano ya kimataifa na kuiwakilisha nchi vema.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

"Michuano ya CAF mwaka huu tunawakilishwa na watani wa jadi, Simba (Klabu Bingwa) & Yanga (Kombe la Shirikisho). Kama alivyowajulisha Msemaji Mkuu wa Serikali, natoa hamasa ya Shilingi Milioni 5 kwa timu hizi mbili kwa kila goli watakalofunga. Tuwakilisheni vyema. Nawatakia kheri" Ameandika Samia katika ukurasa wake wa Twitter akisindikiza ujumbe huo na picha ya vikosi vya Simba na Yanga kama inavoonekana hapa chini;


Klabu ya Simba inakabiliwa na mchezo wake dhidi ya Raja Casablanca utakaochezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18 Februari 2023 katika mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika mchezo utakaochezwa katika dimba la Mkapa (Mkapa Stadium) jijini Dar es Salaam.

Wakati huo Klabu ya Yanga itakuwa na mchezo wake siku ya Jumapili Februari 19, 2023 dhidi ya TP Mazembe mchezo utakaopigwa pia katika uwanja wa Mkapa (Mkapa Stadium) katika mashindani ya kombe la shirikisho la CAF linalijulikana kama Kombe la Shirikisho la TotalEnergies kwa madhumuni ya udhamini.

Post a Comment

Previous Post Next Post