Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa Sheria ya Takwimu Sura 351. Kwa mujibu wa Sheria hiyo, NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji na usambazaji wa Takwimu Rasmi nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za Mfumuko wa Bei kwa ajili ya matumizi ya Serikali na wadau wa takwimu. Mfumuko wa Bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini.

Picha ya Maktaba

Na Mwandishi wetu

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 umeongezeka hadi asillmia 4.9 kutoka asillmia 4.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba, 2022. Hil Inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka uliolshia mwezi Disemba, 2022.

Kuongezeka kwa Mfumukowa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 kumechangiwa na kuongezeka kwa Mfumuko wa bei kwa baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 ikilinganishwa na kipindi cha mwaka ulioishia mwezi Disemba, 2022.

Baadhi ya bidha za vyakula zilizoonesha kuongezeka kwa Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi Disemba, 2022 ni pamoja na;

-  Ngano (kutoka asilimia 6.0 hadi asillmla 7.7)
-  Unga wa mtama (kutoka asillmia 1.0 hadi asillmla 3.9)
-  Samaki (kutoka asilimia 4.2 hadi asilimia 4.3)
-  Matunda (kutoka asilimia 1.9 hadi asilimia 5.5)
-  Mbogamboga (kutoka asllimia 3.6 hadi asilimia 5.2)
-  Viazi vitamu (kutoka asilimia 3.9 hadi asilimia 5.3)
-  Choroko (kutoka asllimia 1.3 hadi asillmia 5.6) na
-  Kunde (kutoka asilimia 8.7 hadi asillmia 13.9).

Kwa upande mwingine, baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kuongezeka kwa Mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 ikilinganishwa na mwaka ulioishia mwezi Disemba, 2022 ni pamoja na;

-  Nguo za wanawake (kutoka asillmia 2.6 hadi asilimia 2.7)
-  Viatu vya wanawake (kutoka asllimia3.4 hadi asilimla 3.5)
-  Vifaa muhimu kwa matumizi ya nyumbani (household appliances) (kutoka asilimia 2.2hadi asillmia 3.5)
-  Dizeli (kutoka asilimla 27.4 hadi asilimia 33.1)
-  Petroli (kutoka asillmia 3.7 hadi asilimia 4.7)
-  Ada za shule (kutoka asillmia 0.7 hadi asillmia 2.9) na huduma ya malazi kwenye hoteli na nyumba zakulala wagenl (guest house) (kutoka asillmia 0.9 hadi asilimla 3.8).

Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za Vyakula na Vinywaji Baridi kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2023 umeongezeka hadi asilimia 9.9 kutoka asilimia 9.7 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba, 2022.

Mfumuko wa Bei ambao haujumuishi bidhaa za Vyakula na Vinywaji baridi kwa mwezi Januari, 2023 umeongezeka kidogo hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 2.9 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba, 2022.


HALI YA MFUMUKO WA BEI KWA BAADHI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KWA MWAKA ULIOISHA MWEZI JANUARI 2023

Nchini Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioisha mwezi Januari, 2023 umeongezeka hadi asilimia 10.4 kutoka asilimia 10.2 kwa mwaka uluoisha Disemba, 2022. Kwa upande wa Kenya, mfumuko wa bei kwa mwaka ulioisha mwezi Januari, 2023 umepungua hadi asilimia 9.0 kutoka asilimia 9.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Disemba , 2022


Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)

Post a Comment

Previous Post Next Post