Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Remidius Mwema amesema watu 12 wamefariki dunia na majeruhi wakiwa 63 kwenye ajali ya basi na lori wilayani Kongwa. 


Akizungumzia ajali hiyo, Mwema amesema tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Sirwa, Kata ya Pandambili wilayani Kongwa, na kusababisha vifo 12, wanaume 8 na wanawake 4.  

Mwema amesema majeruhi wa ajali hiyo ni 63, wanaume 40 na wanawake 23.  Ajali hiyo imehusisha basi la Frester lililokuwa likitokea Bukoba mkoani Kagera kwenda Dar es Salaam baada ya kugongana na lori uso kwa uso katika Kijiji cha Sirwa usiku wa kuamkia leo. 


Amesema majeruhi 36 wapo katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo na wanne wamepelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kuonekana wana matatizo makubwa. 

Amesema majeruhi 27 walipelekwa katika kituo cha Afya cha Kibaigwa ambapo kati ya hao, 16 walihamishiwa Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu zaidi.

Post a Comment

Previous Post Next Post