Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohane [St. John] Alicia Mwami akitoa tuzo kwa watumishi Wizara ya Afya ,aliyevaa koti jeusi ni Afisa Mpango wa Taifa, huduma za Afya ngazi ya Jamii, Mwailafu Bahati akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi  Wizara ya Afya, idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Dkt. Tumaini Haonga  na watumishi wengine kwa niaba ya Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa ufanisi wa kazi.


Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohane [St.John] Dodoma, kimetoa Tuzo ya pongezi  kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwa kuwa mstari wa mbele kuiongoza vyema Wizara katika masuala mbalimbali ya afua za Afya.


Akizungumza mara baada ya kutoa tuzo hiyo katika hafla ya ‘’Afya Day “iliyotolewa  mbele ya  watumishi wa Wizara ya Afya akiwemo Kaimu Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, idara ya Kinga Wizara ya Afya ,Dkt. Tumaini Haonga, Afisa Mpango wa Taifa, huduma za Afya ngazi ya Jamii, Mwailafu Bahati, Rais wa chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohane [St. John] Alicia Mwami amesema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amekuwa Waziri wa Mfano wa kuigwa hapa nchini katika kuhakikisha Elimu ya Afya inafika kwa kila jamii ya kitanzania juu ya tahadhari ya Magonjwa.


“Tumejionea Waziri wa Afya Ummy Mwalimu anavyopambana kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uelewa juu ya Masuala mbalimbali ya Afya hivyo kama serikali ya Wanafunzi chuo kikuu cha St. John tumeamua kutoa tuzo maalum kwa ajili ya Waziri Ummy” amesema Alicia.


Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi  Wizara ya Afya, idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Dkt. Tumaini Haonga  akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohane [St. John] Alicia Mwami baada ya kutoa tuzo ya pongezi kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu iliyosema "Tuzo ya Pongezi kwa Mhe. Ummy Mwalimu kwa kusimamia vizuri sekta ya Afya, tunakutakia utekelezaji mwema katika majukumu yako”


Kwa upande wake Kaimu Mkurungezi Sehemu ya Elimu ya Afya  kwa Umma, Wizara ya Afya Dkt. Tumaini Haonga amesema ataenda kuiwasilisha vyema tuzo hiyo kwa Waziri Ummy Mwalimu.


Ikumbukwe kuwa "Afya Day "Chuo Kikuu cha St.John imeratibiwa na Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambapo imekwenda sambamba na kaulimbiu isemayo "Nachukua hatua Stahiki za Kinga dhidi ya Magonjwa, kufanya uchunguzi wa Afya wa awali mara kwa mara na kuwahi  huduma za matibabu ili kuendeleza afya yangu"


Kaimu Mkurugenzi  Msaidizi  Wizara ya Afya, idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma, Dkt.Tumaini Haonga pamoja na Afisa Mpango wa Taifa, huduma za Afya ngazi ya Jamii, Mwailafu Bahati na watumishi wengine Wizara ya Afya, Idara ya Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma wakiwa katika picha ya pamoja wanafunzi wa serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohane [St. Yohane] katika kuhitimisha hafla ya “Afya Day” chuoni hapo.

Post a Comment

Previous Post Next Post