Imeelezwa kwamba wiki ya sheria ambayo huwa inaadhimishwa kila mwaka ina lengo la kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayohusu sheria, migogoro na mambo yanayohusu utafutaji wa haki mahakamani.

Hayo yameelezwa na hakimu mkazi mfawidhi mahakama ya hakimu mkazi Lindi C.P Consolata Singano wakati akizungumza na Mashujaa FM kuhusu ufunguzi wa wiki ya sheria mkoa wa Lindi ambayo imeanza hapo jana.

Akizungumzia suala la usuluhishi Amedei Mkoba ambaye ni msuluhishi na muamuzi mfawidhi kutoka tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) mkoa wa Lindi amesema uelewa kuhusu suala la usuluhishi mkoa wa Lindi liko chini.

Post a Comment

Previous Post Next Post