YOUR FUTURE IS CREATED BY WHAT YOU DO TODAY, NEVER TOMORROW




Na Faustine Gimu (Elimu ya Afya Kwa Umma, Kilimanjaro)

Wataalam wa Afya kutoka kanda ya Kaskazini inayounda mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga wameweka maazimio ya pamoja yatakayorahisisha kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga.

Wakitoa maazimio hayo katika kikao cha kanda ya Kaskazini cha kujadili vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kilichoandaliwa na Wizara ya Afya baadhi ya wataalam hao akiwemo Raphael Mumba kaimu Mganga mkuu mkoa wa Tanga,Sinpho Siale Muuguzi mfawidhi Hospitali ya Mount Meru pamoja na Dkt. Glory Mangi Daktari Bingwa magonjwa ya mama na uzazi hospitali ya Rufaa Kilimanjaro,KCMC wamesema lengo la maazimio hayo ni kupunguza zaidi vifo.


Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto Kanda ya Kaskazini Haikamesia Malisa amesema maazimio ya kikao hicho cha siku mbili  itakuwa kipimo kitakachokuwa kinapimwa kwa kila robo mwaka katika utekelezaji huku mwakilishi wa Mganga Mkuu mkoa wa Kilimanjaro Dkt.Andrewleon Saashisha Quaker akisema wataenda kutekeleza maazimio hayo.

Afisa Programu  Wizara ya Afya,Idara ya Afya ya Uzazi,mama na Mtoto Jackline Ndanshau amesema ni muhimu kutekeleza maazimio  hayo.

Post a Comment

Previous Post Next Post