Katika mji wa kusini wa Arequipa, waandamanaji takriban 1,000 walijaribu kuvamia uwanja wa ndege siku ya Alhamis, lakini walizuiliwa na polisi waliofyatua mabomu ya machozi. Waandamanaji hao ambao wamesambaa katika mji mkuu wakitokea kwenye mikoa mbalimbali walilenga kufika kwenye ikulu yenye ulinzi mkaali hapo jana Alhamis.
Mmoja wa waandamanaji amekaririwa na vyombo vya habari akisema maandamano hayo yanalenga kupigania haki yao ya kidemokrasia.
Rais wa Peru Dina Boluarte Katika hotuba yake iliofuatiliwa kwa ukaribu na waandamanaji wakitaka kujua kama wamejibu hoja zao amesema hakuna faida katika maandamano hayo yaliyosababisha machafuko na kuyataja ni kinyume cha sheria. "Mnadai madai nje ya utawala wa sheria mkitaka kuiondoa serikali." Amesema Bi. Boluarte
Bi Boluarte, mwanasheria mwenye umri wa miaka 60, ni C, ikiwa tangu ipate uhuru wake zaidi ya miaka 200 iliyopita. Pia amesema anaunga mkono uchaguzi wa Rais na wabunge kufanyika 2024 ikiwa hapo awali ulipangwa 2026.
Post a Comment